Timu ya taifa ya Uganda ya mchezo wa Kriketi, leo inacheza na timu ya Vanuatu katika mashindano ya dunia ya mchujo wa awalli yanayondelea nchini Malaysia.
Uganda ambayo ilipata matumaini ya kusonga mbele baada ya kuifunga Bermuda siku ya jumatatu kwa mikimbio (runs) 189, italazimika kushinda ili kujiweka katika mazingira mazuri zaidi ya kufuzu.
Katika mchezo wake wa kwanza nchini Malaysia, Uganda ilifungwa na wenyeji kwa mikimbio (runs) 9.
Katika mechi hizo za mchujo timu mbili kati ya 6 zinazoshindana nchini Malaysia, zitafuzu mashindano ya dunia ya daraja la juu mwaka huu.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |