• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la Usalama la UM lalaani shambulizi la mabomu Kabul

    (GMT+08:00) 2018-05-02 10:20:23

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa taarifa kulaani vikali shambulizi la mabomu lililotokea jumatatu mjini Kabul, Afghanistan na kusababisha vifo vya watu 41, na wengine 45 kujeruhiwa.

    Taarifa imesema wajumbe wa baraza hilo wameeleza kusikitishwa na tukio hilo, kutoa rambirambi kwa familia za wafiwa na kuwatakia majeruhi wapone haraka.

    Taarifa hiyo imesisitiza kuwa ni lazima watendaji, wapangaji, wafadhili, na wanaounga mkono vitendo vya kigaidi kama hivyo wafikishwe mbele ya sheria, na nchi zote zinapaswa kushirikiana na serikali ya Afghanistan na makundi mbalimbali nchini Afghanistan, kwa kufuata sheria za kimataifa na maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako