• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mtu mmoja auawa na mwingine kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la risasi jijini London

  (GMT+08:00) 2018-05-02 18:06:54

  Vyombo vya habari mjini London, Uingereza, vimesema mtu mmoja ameuawa na mwingine kujeruhiwa vibaya katika shambulizi la risasi lililotokea jana usiku kaskazini magharibi mwa mji wa London.

  Mtu huyo alikutwa na majeraha makubwa nje ya kituo cha treni cha Queensbury majira ya saa tatu usiku kwa saa za huko, na alifariki katika eneo hilo saa moja baada ya polisi na wahudumu wa afya kuwasili barabara ya Cumberland ambapo shambulizi la risasi lilitokea. Majeruhi amepelekwa hospitali, na hali yake inaendelea vizuri.

  Hakuna taarifa zozote kuhusu utambulisho wa mtu aliyefanya mauaji hayo, na polisi wanachunguza picha za CCTV katika eneo hilo ili kuweza kupata chanzo cha shambulizi hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako