• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakenya wazidi kuathirika na kupanda kwa gharama za maisha

    (GMT+08:00) 2018-05-02 19:20:57

    Wakenya jumanne waliadhimisha siku ya wafanyakazi duniani huku gharama ya maisha ikiendelea kupanda na kuathiri uchumi kwa kiasi kikubwa.

    Katibu Mkuu wa vyama vya wafanyakazi Ndugu Francis Atwoli alihusisha hali hiyo na sera hafifu za serikali,ufisadi na mazingira ya kisiasa yaliyoshuhudiwa wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2017.

    Aidha Atwoli alisema kuwa kuna matumaini mazuri ya uchumi kufufuka baada ya muafaka kati ya Rais Uhuru Kenyatta na kiongozi wa uoinzani Raila Odinga.

    Alisema kutokana na hali ngumu ya maisha,wakenya wamekuwa wakihamia mataifa ya milki za kiarabu kama Qatar na Saudi Arabia kusaka ajira,ambako huwa wanadhulumiwa na kuteswa na waajiri wao na hata kuuawa.

    Kwenye hotuba yake iliyosomwa na Waziri wa Leba Ukur Yattani,Rais Uhuru Kenyatta aliongeza mishahara ya wafanyakazi wa viwango vya chini kwa asilimia tano.

    Nyongeza hiyo ilijiri hata baada ya baadhi ya waajiri kutii agizo la serikali mwaka jana la kuongeza mishahara ya chini kwa asilimia 18.

    Bw Yattani alisema kwamba atashirikiana na viongozi wa vyama vya wafanyakazi kuimarisha mazingira ya kufanyia kazi nchini.

    Afisa Mkuu Mtendaji wa Shirikisho la Waajiri nchini (FKE), Bi Jackline Mugo alisema hali ni mbaya hivi kwamba maelfu ya Wakenya wanaendelea kupoteza kazi kila mwaka.

    Alisema zaidi ya Wakenya 10,000 walipoteza ajira katika sekta ya benki pekee mwaka jana na kuongeza kuwa ipo haja ya kuhakikisha Wakenya wanapata kazi zitakazowahakikishia maisha mema siku za baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako