• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matayarisho ya Maonesho ya Kimataifa ya Biashara Rwanda (RITF) yameanza

    (GMT+08:00) 2018-05-02 19:21:46

    Matayarisho kwa ajili ya maonesho ya Kimataifa ya Biashara Rwanda mwaka 2018 (RITF) tayari yameanza.

    Maonesho hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la Sekta Binafsi yanatarajiwa kuanza tarehe 26 Julai hadi 15 Agosti katika viwanja vya maonesho vya Gikondo mjini Kigali.

    Akizungumza na gazeti moja la Rwanda,Mkuu wa Mawasiliano na Masoko wa Shirikisho la Sekta Binafsi, Eric Kabeera, alisema maonesho hayo yanatarajia kuvutia biashara zaidi ya 500 kutoka nchi 20 duniani.

    Alisema maonesho hayo ya kila mwaka yatahusisha sekta mbalimbali zikiwemo,mawasiliano na teknolojia,kilimo biashara,viwanda,ujenzi na nguo.

    Alisema nia ni kutengeneza jukwaa la kuwaunganisha wawekezaji wa Rwanda na wenzao wa kigeni ili kusaidia kutafuta soko kwa ajili ya bidhaa za ndani ,na kuboresha ushindani wao.

    Waandaaji wanasema maonesho hayo pia yatatumika kama jukwaa la kuvutia makampuni ya kigeni kuwekeza nchini Rwanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako