• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Tanzania kuajiri walimu zaidi ya 10,000 wa shule za msingi

  (GMT+08:00) 2018-05-03 09:01:56

  Serikali ya Tanzania imesema itaajiri walimu zaidi ya 10,000 wa shule za msingi kabla ya tarehe 30 mwezi Juni, ili kujaza pengo la walimu linaloikabili nchi hiyo.

  Naibu waziri wa nchi anayeshughulikia utawala wa mikoa na serikali za mitaa Bw. Joseph Kakunda, ameliambia bunge huko Dodoma kuwa serikali ya Tanzania inafanya juhudi ili kutatua suala la upungufu wa walimu.

  Bw. Kaunda amesema serikali inashirikiana kwa karibu na Baraza la mitihani la Taifa kupitia vyeti vya walimu, na inatarajia kuajiri walimu 10,140 kabla ya mwisho wa mwezi Juni mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako