Rais Xi Jinping wa China ametoa mwito wa kujenga vyuo vikuu vya kisasa vyenye umaalum wa China, ili kuwalea watu kujiunga na mkondo wa ujamaa.
Rais Xi Jinping amesema hayo alipofanya ziara ya ukaguzi katika chuo Kikuu cha Beijing, kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya vijana ya China na maadhimisho ya miaka 120 ya chuo kikuu cha Beijing, ambayo yote yameangukia leo tarehe 4 Mei.
Baada ya kufahamishwa kuhusu mafanikio ya hivi karibu ya chuo Kikuu cha Beijing kwenye mambo ya utafiti na uhandisi, Rais Xi alikumbusha kuwa uvumbuzi ni injini kuu ya maendeleo, na sehemu muhimu ya nguvu ya taifa na kiini cha ushindani.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |