• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafungua soko la magari kunufaisha mashirika ya nchi za nje

    (GMT+08:00) 2018-05-03 16:48:55

    Hivi karibuni China imechukua hatua mbalimbali za kufungua soko la magari, ikiwemo kupunguza masharti ya kumiliki hisa ya mashirika ya magari nchini China kwa wawekezaji wa nchi za nje, na kupunguza ushuru wa forodha kwa magari yanayoagizwa kutoka nje kwa kiasi kikubwa. Hali hii imefuatiliwa na nchi za nje. Wataalamu wanaona China kufungua soko lake la magari kutanufaisha nchi za nje, na pia kunayahimiza mashirika ya magari ya ndani kujiendeleza zaidi.

    Tangu China itangaze kufungua mlango zaidi kwenye mkutano wa baraza la Asia la Boao, China imeharakisha kufungua masoko yake kwa mashirika ya nchi za nje. Msemaji wa wizara ya viwanda na habari ya China Bw. Chen Yin, amesema katika siku zijazo China itafungua soko lake la magari kwa kiasi kikubwa. Anasema,

    "Mwaka huu, China itaondoa masharti ya kumiliki hisa ya makampuni yanayotengeneza magari maalumu na magari yanayotumia nishati safi nchini China kwa wawekezaji wa nchi za nje, mwaka 2020 China itaondoa masharti hayo kwa mashirika ya magari ya kibiashara, na mwaka 2022 masharti hayo yataondolewa katika mashirika ya magari ya aina zote, pia sharti kwamba shirika moja la nje linaweza kuanzisha makampuni mawili nchini China litaondolewa."

    Wataalamu wanaona China kufungua soko la magari kwa nchi za nje, ni chaguo la kutimiza ustawi wa pamoja. Mchambuzi wa sekta ya magari Bw. Jia Xinguang anasema,

    "Kwa Mfano hatuna uwezo wa kutosha katika utafiti wa baadhi ya teknolojia muhimu, huku tukikabiliwa na changamoto ya maendeleo ya magari yanayotumia nishati safi. Badala ya kujilinda, kufungua soko kutatusaidia zaidi. Pia ushindani utahimiza maendeleo ya mashirika yetu ya magari."

    Bw. Jia anaona kupunguza ushuru wa forodha kwa magari yanayoagizwa kutoka nje na kuondoa masharti ya kumiliki hisa ya mashirika ya magari nchini China kwa wawekezaji kutoka nchi za nje, kutalazimisha mashirika ya magari ya China kufanya juhudi zaidi ili kujiendeleza. Anasema,

    "Hivi karibuni China ilipunguza kodi kwa sekta za uzalishaji viwandani, pia ilipunguza ushuru wa forodha kwa magari yanayoagizwa kutoka nje na kuondoa masharti ya kumiliki hisa ya mashirika ya magari nchini China kwa wawekezaji wa nchi za nje. Hatua hizo zitaleta ushindani mkubwa zaidi kwa mashirika ya magari ya China. Ushindani huo utaangamiza mashirika dhaifu na kuendeleza mashirika bora. Hivi sasa tuna mashirika mengi kupita kiasi ya kutengeneza magari, lakini hakuna mashirika ya kutosha yenye nguvu ya kushindana na mashirika ya nchi za nje. Tunatumani kuwa hatimaye tutakuwa na mashirika makubwa ya kimataifa."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako