• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yakaribisha nchi zote zijiunge na Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja"

    (GMT+08:00) 2018-05-03 18:00:31

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bibi Hua Chunying amesema, China inazikaribisha nchi nyingi zaidi kujiunga na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" ambalo tangu litolewe miaka mitano iliyopita, nchi na sehemu nyingi zaidi zimenufaishwa kutokana na pendekezo hilo..

    Kamati ya kuhimiza uhusiano kati ya New Zealand na China iliyoko nchini New Zealand imetangaza ripoti ya utafiti kuhusu pendekezo hilo, na kusema litatoa fursa nyingi, na kama New Zealand haitajiunga nalo kwa wakati, basi itapoteza fursa nzuri.

    Akizungumzia ripoti hiyo Bibi Hua Chunying amesema, hadi sasa nchi na sehemu zaidi ya 80 duniani zimesaini makubaliano ya ushirikiano na China. Kuanzia mwaka 2013 hadi 2017, thamani ya jumla ya biashara kati ya China na nchi zinazojiunga na pendekezo hilo imefikia RMB trilioni 33.2, sawa na dola za kimarekani trilioni 5.23, ikiwa ni ongezeko la asilimia 4 kwa mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako