• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Benin ahimiza uhusiano kati ya nchi hiyo na China

  (GMT+08:00) 2018-05-04 18:31:23

  Rais Patrice Talon wa Benin amesema anapenda kuhimiza uhusiano kati ya nchi hiyo na China ufikie kwenye kiwango kipya.

  Rais Talon amesema hayo jana alipokuwa akipokea hati za utambulisho wa balozi mpya wa China nchini Benin Bw. Peng Jingtao. Amesema Benin inaichukulia China kuwa mshirika wa kimkakati, na maendeleo ya uchumi na jamii ya Benin hayawezi kukosa ushiriki na uungaji mkono wa China. Pia amesema nchi yake inaishukuru sana China na inatarajia ushirikiano kati ya pande hizo mbili upate mafanikio makubwa zaidi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako