• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Barafu nyingi huenda ziko chini ya ardhi ya mwezi

    (GMT+08:00) 2018-05-07 16:15:02

    Watafiti wa Chuo Kikuu cha Kaskazini Mashariki cha Japan wamesema wamegundua madini kwenye miamba ya mwezi, ambayo inaonesha kuwa huenda kuna barafu nyingi chini ya ardhi ya mwezi. Na kama makisio haya yakithibitishwa, kituo kitakachojengwa kwenye mwezi kitaweza kuzalisha maji ya kunywa na nishati ya Hydrogen kwa barafu hizi.

    Watafiti hao wametoa tasnifu kwenye jarida la Science Advances la Marekani ikisema wamechambua miamba ya mwezi iliyoanguka barani Afrika katika miaka elfu 17 iliyopita, na kugundua madini ya Moganite, ambapo yanapoundwa yanahitaji maji mengi.

    Watafiti wamekadiria kuwa kuna lita 18.8 ya maji kwenye mita 1 ya ujazo ya miamba iliyoko chini ya ardhi ya mwezi, na maji hayo huenda yanaganda.

    Watafiti wamesema kabla ya hapo watafiti walifikiri maji au barafu zipo kwenye ncha mbili za mwezi, na utafiti mpya unaonesha kuwa maji huenda pia yako kwenye sehemu nyingine mwezini, na jambo hili ni muhimu kwa uendelezaji wa mwezi katika siku zijazo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako