• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatoa wito kuthamini hali iliyopatikana kwa juhudi kubwa katika Peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2018-05-08 10:35:28

    Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China Bw. Geng Shuang ametoa wito kwa pande husika kuthamini hali ya sasa ya Peninsula ya Korea iliyopatikana kwa juhudi kubwa, ili kudumisha utulivu na mwelekeo mzuri.

    Bw. Geng Shuang amesema hayo baada ya Korea Kaskazini kuishutumu Marekani kupotosha na kuharibu hali nzuri ya mazungumzo ambayo ilipatikana baada ya juhudi kubwa.

    Marekani inaona hatua ya Korea Kaskazini ya kutangaza kuacha mpango wake wa nyuklia kupitia makubaliano ya Panmunjom inatokana na vikwazo na shinikizo.

    Bw. Geng Shuang anatumai kuwa mazungumzo yanayopangwa kufanyika kati ya viongozi wa Korea Kaskazini na Marekani, yatafanyika kwa utaratibu na kuwa na matokeo mazuri, na mwelekeo mzuri wa hali ya Peninsula ya Korea uitaimarishwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako