• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Uganda na Tanzania zakubaliana kuongeza kasi ya ujenzi wa bomba la mafuta

    (GMT+08:00) 2018-05-08 17:16:00

    Uganda na Tanzania zimekubaliana kuongeza zaidi kasi ya ujenzi wa bomba la mafuta kati ya Hoima na bandari ya Tanga.

    Mawaziri wa kawi wa nchi hizo mbili pamoja na wakuu wa sheria walikutana mjini Kampala kwa majadiliano yanayoendela kuhusu mradi huo wa dola bilioni 3.5.

    Licha ya marais wa nchi hizo mbili kuagiza kuharakishwa kwa ujenzi wa bomba hilo, bado kuna maswala kadhaa ya kisheria ambayo hayajakamilishwa.

    Wakati huo huo serikali ya Uganda imesaini miradi 11 ya dola bilioni 2.8 inayohusiana na usimamizi na ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta kwenye eneo la hoima.

    Miradi hiyo inayohusisha Uganda na kampuni za marekani itawezesha kufunguliw akwa nafasi 5,000 za ajira.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako