• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kombe la dunia kwa watoto: Timu ya Tanzania yaondoka kuelekea Russia

  (GMT+08:00) 2018-05-10 09:21:52

  Rais wa shirikisho la miguu Tanzania (TFF) Wallace Karia jana ameiaga timu ya watoto wa kituo cha watoto wenye mazingira magumu cha TSC cha jijini Mwanza wanaokwenda nchini Russia kwenye kombe la dunia kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu.

  Timu hiyo imeondoka na wachezaji 9 na viongozi 4 kutimiza jumla ya watu 13 kwenye msafara wao.

  Rais wa TFF Karia, ameitakia heri timu hiyo na kuhakikisha inapeperusha vyema bebdera ya Tanzania kwenye michuano hiyo. Mwaka 2014 timu hiyo ilifanikiwa kutwaa kombe la dunia kwenye michuano kama hiyo iliyofanyika nchini Brazil.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako