• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU kuisaidia DRC kudhibiti mlipuko mpya wa Ebola

    (GMT+08:00) 2018-05-11 14:11:19

    Kituo cha kudhibiti na kuzuia magonjwa cha Afrika (Afrika CDC) kimeanzisha operesheni ya dharura ya kuunga mkono juhudi za Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC katika kupambana na mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola nchini humo.

    Serikali ya DRC imetangaza kuibuka tena kwa Ebola Jumanne wiki hii, baada ya sampuli mbili kuthibitishwa kuwa na virusi vya ugonjwa huo EVD mkoani Equateur nchini humo.

    CDC Afrika itatuma timu ya kudhibiti milipuko ya magonjwa ambayo itajumuisha wataalamu wenye uzoefu wa kukabiliana na Ebola ilipolipuka mwaka 2014 katika Afrika Magharibi na mwaka 2017 nchini DRC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako