• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya yawataka wanakandarasi kujenga mabwawa kwa kuzingatia viwango bora vya kiufundi

    (GMT+08:00) 2018-05-11 19:21:11

    Naibu Rais William Ruto amewataka wakandarasi wa kujenga mabwawa kuzingatia viwango vya kiufundi vilivyoidhinishwa ili kuzuia mikasa inayosababisha na utendakazi mbovu. Ruto amesema mabwawa yanapaswa kujenga kwa kuzingatia kiwango cha juu cha utaalamu ili kuzuia mikasa kama iliyotokea kule Nakuru. Bw Ruto ameamuru idara husika kuhakikisha kuwa mabwawa yaliyosalia yanatunzwa vizuri kwa kuzingatia teknolojia ya kisasa.Taarifa hii inakuja siku mbili tu baada ya mkasa wa hivi punde ambapo ukuta wa Bwawa la Patel lililoko Solai Nakuru lilivuja maji na kusababisha vifo vya watu wengi. Bw Ruto alisema mikasa kama hii inaweza kukomeshwa kupitia utendakazi mzuri. Wizara ya Maji imesema mabwawa 141 madogo yamejengwa kote nchini, huku asilimia 90 ya mabwawa hayo yamejaa maji wakati huu ambapo mvua inshuhudiwa kwa wingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako