Meli ya pili inayobeba ndege za kivita ya China leo imefunga safari kutoka bandari ya viwanda vya utengenezaji wa meli ya Dalian na kufanyiwa majaribio ya mfumo wa injini na vifaa vyingine.
Habari zinasema kuwa, kazi ya utengenezaji wa meli hiyo imeendelea kufuatia mpango uliopangwa baada ya terehe 26 Aprili mwaka jana ilipozinduliwa, na kukamilisha shughuli ya kubaini kasoro, kufanya marekebisho ya mfumo na vifaa, utengenezaji na majaribio husika ya nanga, na hatimaye sasa imekuwa na hali ya kiufundi ya kwenda baharini kufanyiwa majaribio.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |