Shirika la afya duniani WHO, limesema kukabiliana na ugonjwa wa ebola ulioibuka hivi karibuni nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC ni changamoto yenye hatari, ugumu na gharama kubwa ambayo inahitaji maandalizi na utayari kwa kila hatua.
Mkurugenzi Mkuu wa WHO Dr. Tedros Ghebreyesus anatarajiwa kusafiri kwenda DRC ili kujionea hali ilivyo na kuongoza mwitikio wa kusaidiana mamlaka za afya za kitaifa.
Siku nne zilizopita kulizuka ugonjwa wa Ebola katika ukanda wa kiafya wa Bikoro, katika jimbo la Ikweta, na hadi kufikia siku ya ijumaa iliyopita kulikuwa tayari na taarifa ya watu 34 waliodhaniwa kuambukizwa, wakiwemo wawili waliyothibitika, 18 kukiwa na uwezekano kuwa wamefariki na wengine 14 wakihofiwa kuwa wameathirika. Sampuli tano zilizochukuliwa kutoka kwa wagonjwa watano na uchunguzi wa maabara ukionyesha kuwa wawili wanao ugonjwa huo.
Lakini mpaka sasa, WHO haijashauri kutolewa katazo kwa watu kutosafiri kwenda DRC au kufanya biashara DRC.
Ugonjwa wa Ebola uliikumba Afrika kati ya mwaka 2013 na 2016, na kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa ulisababisha vifo vya hadi watu 11,000 kati ya 30,000 waliyoambukizwa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |