• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" lapata mafanikio makubwa katika miaka mitano iliyopita

  (GMT+08:00) 2018-05-14 18:38:15

  Pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" lililotolewa na China miaka mitano iliyopita limepata mafanikio makubwa, nchi na sehemu mbalimbali, mashirika na makampuni mengi yameitikia vizuri pendekezo hilo na kushiriki kwa kina.

  Hadi kufikia mwezi Aprili mwaka huu, China imesaini makubaliano 101 ya ushirikiano wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" na nchi na mashirika ya kimataifa 86, ambayo yanahusu sekta za miundo mbinu, uzalishaji, uwekezaji, uchumi na biashara, mambo ya fedha, sayansi na teknolojia, jamii na sekta nyingine.

  Katika miaka mitano iliyopita, thamani ya jumla ya biashara kati ya China na nchi husika za "Ukanda Mmoja na Njia Moja" imezidi dola za kimarekani trilioni 5. Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti ya "Ukanda Mmoja na Njia Moja" katika chuo kikuu cha ualimu cha Beijing Bw. Hu Biliang anasema, chanzo cha kimsingi cha mafanikio ya pendekezo hilo ni kwamba, si kama tu linahimiza maendeleo ya kina ya China, bali pia linaweza kusukuma mbele maendeleo zaidi ya dunia.

  "Mwaka 2013, pendekezo la 'Ukanda Moja na Njia Moja' lilipotolewa ilikuwa ni kipindi cha kudidimia kwa uchumi wa dunia nzima. Pendekezo hilo limehimiza ongezeko la uwekezaji, matumizi na ongezeko la nafasi za ajira kwa kupitia ujenzi wa miundombinu na mawasiliano, na kuongeza kipato zaidi kwa nchi husika, kuhimiza ongezeko la uchumi duniani hasa nchi zinazoendelea, kutia nguvu mpya kwa maendeleo ya uchumi ya nchi zinazoendelea, na kutia motisha mpya kwa ongezeko la uchumi duniani."

  Wachambuzi wanaona kuwa, ujenzi wa "Ukanda Mmoja na Njia Moja" unasaidia kutatua kukwama kwa utandawazi wa uchumi duniani, kuhimiza uchumi wa dunia uwe na uwiano, shirikishi zaidi na maendeleo endelevu. China inaharakisha kuhimiza hali mpya ya kufungua mlango kwa pande zote, na kunufaisha uchumi wa dunia nzima.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako