• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marekani kuondoa vikwazo vya uchumi dhidi ya Korea Kaskazini kama nchi hyo ikiacha silaha za nyuklia

  (GMT+08:00) 2018-05-14 19:31:49

  Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Bw. Mike Pompeo amesema kama Korea Kaskazini ikiweza kutimiza kutokuwa na silaha za nyuklia, Marekani itaondoa vikwazo dhidi ya nchi hiyo na kuyaruhusu makampuni binafsi ya Marekani kuwekeza nchini humo.

  Bw. Pompeo amesema hayo jana katika kipindi cha telivisheni cha Shirika la matangazo ya Columbia, pia amesema Marekani itaisaidia Korea Kaskazini kupata ustawi wa uchumi.

  Aidha Bw. Pompeo alipohojiwa na waandishi wa habari wa Shirika la Fox News amesema hiyo inamaanisha kuwa makampuni binafsi ya Marekani yataisaidia Korea Kaskazini katika sekta za nishati, ujenzi wa miundombinu na kilimo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako