• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kaunti ya Kajiado yaweka vifaa vya kisasa katika nyumba za jadi za wamasai,Manyatta kwa ajili ya kujifungua

    (GMT+08:00) 2018-05-15 09:19:05

    Hospitali ya kisasa ambayo itasaidiwa na nyumba za kijadi za wamasai yaani manyatta imefunguliwa katika kaunti ya Kajiado nchini Kenya.

    Jukumu kubwa la manyatta ni kuwavutia wanawake wa kimasai kujifungua watoto wao hospitalini.Kwa kawaida wanawake wa kimasai hujifungua nyumbani chini ya usimamizi wa wakunga wa jadi.

    Ni katika kijiji cha Ngatataek mjini Kajiado ambapo hospitali ya kisasa pamoja na manyatta zimejengwa ili kuwashughulikia wamama wajawazito.Nyumba hii ndogo ya kijadi ya wamasai inayojengwa kwa tope na nyasi,ambayo inajulikana kama manyatta ina umuhimu mkubwa hapa.

    Lengo la nyumba hii ni kuokoa maisha ya wanawake wajawazito katika eneo la Kajiado.

    Manyatta hii imejengwa kando ya hospitali ya kisasa ya kina mama wajawazito kujifungua.Imejengwa hapa mahsusi ili kuvutia wanawake wa kimasai kujifungua hospitalini,kwa sababu miko na tamaduni za wamasai haziruhusu hivyo.

    Kwa sababu wanawake wa kimasai wamezoea kujifungua nyumbani ndani ya manyatta zao,manyatta hii imejengwa ili kufanya kazi hiyo,tofauti iliyopo ni kuwa hapa kuna madaktari na manesi waliohitimu.

    Manyatta hii inatumika kama eneo ambalo wamama wajawazito walio na uchungu wanasubiri kabla kujifungua,na kuleta ile mandhari ya kuwa nyumbani.Manyata hii pia inatumika kama eneo la kupumzika baada ya kujifungua salama.

    Agnes Tuiye ni mama mjamzito aliyekuja kujifungua katika manyatta hii.

    "Hii manyatta ni nzuri kwa sababu iko na joto.Ukikaka hapa unajihisi kama uko nyumbani kwako kwa sababu tunaishi katika nyumba kama hii.Nilikuja hapa na mkunga tunakaa nay eye lakini daktari anakuja kuniangalia.Nakaa hapa nikipumzika,Napata chakula.Najisikia niko nyumbani,natembeatembea nikirudi kwa kitanda".

    Waziri wa Afya katika kaunti ya Kajiado Bi Esther Somoire anasema hospitali hiyo mpya ya Ngatataek pamoja na manyatta zitahudumia watu wengi zaidi.

    "Kituo hiki kitahudumia watu wengi,na kutoa huduma bora zaidi".

    Kutokana na masuala ya mila na faragha,wanawake wengi wa kimasai hawaendi hospitali kujifungua,jambo linalosababisha vifo vya watoto na wanawake wengi wakati wa kujifungua.

    Hata hivyo kutokana na kufunguliwa kwa kituo hiki,hali hii inatarajiwa kubadilika kwa sababu wanawake wengi sasa wanaenda kujifungua katika manyatta iliyojengwa ambapo wanapata usaidizi na matibabu kutoka kwa madaktari,kama anavyoeleza Bi Rachel Sien,mama aliyejifungua katika kituo hiki.

    "Wamama wengi sana wanapenda hapa kwa manyatta kwa sababu kuna joto .Watoto wnapata joto,ni pazuri.Madaktari wanpokea watu vizuri"

    Wakunga wa jadi ndio wanaowashughulikia wanawake wajawazito ndani ya manyatta.Wakati mama akiwa karibu kujifungua,wakunga huwaita manesi ambao huwahamisha wajawazito katika kituo cha kisasa kwa ajili ya kujifungua.

    Baada ya kujifungua salama,mzazi hurudishwa katika manyatta ambapo anapata uangalizi wa karibu kutoka kwa manesi na wakunga wa jadi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako