• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ubalozi wa Marekani wazinduliwa Jerusalem kukiwa na upinzani mkali duniani

    (GMT+08:00) 2018-05-15 09:59:39

     

    Ubalozi mpya wa Marekani nchini Israel umezinduliwa rasmi mjini Jerusalem, licha ya upinzani mkali kutoka kwa Wapalestina na nchi nyingine nyingi.

    Raia wengi wa Palestina jana waliandamana katika sehemu mbalimbali nchini humo na kupambana na wanajeshi wa Israel, ambapo wapalestina 55 waliuawa na wengine zaidi ya 2,800 kujeruhiwa. Idadi hiyo ya vifo vya Wapalestina inasemekana kuwa ni kubwa zaidi kutokea ndani ya siku moja tangu vita vya Gaza vitokee mwaka 2014.

    Katika hotuba aliyoitoa kwa njia ya video, rais Donald Trump wa Marekani alisema Marekani ingehamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Jerusalem mapema, na kuongeza kuwa nchi hiyo itaendelea kuhimiza makubaliano ya amani ya kudumu kati ya Israel na Palestina.

    Serikali za nchi mbalimbali zikiwemo Ufaransa, Russia, Iran, Syria, Misri, Afrika Kusini zimelaani na kuipinga Marekani kuhamisha ubalozi wake na pia kutoa mwito kwa Israel kujizuia katika kutumia nguvu.

    Na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kufanya mkutano wa dharura kushughulikia mapambano yaliyotokea kati ya waandamanaji wa Palestina na wanajeshi wa Israel katika ukanda wa Gaza karibu na mpaka wa Israel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako