• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Klabu Bingwa Afrika: KCCA ya Uganda kuikaribisha Al Ahly ya Misri mjini Kampala

  (GMT+08:00) 2018-05-15 10:08:19

  Leo ni leo mjini Kampala katika uwanja wa Mandela ambapo wawakilishi pekee wa Afrika Mashariki kwenye hatua ya makundi ya klabu bingwa Afrika KCCA ya Uganda, wanacheza dhidi ya mabingwa wa kihistoria Al Ahly ya Misri.

  Mechi hiyo itapigwa saa kumi kwa saa za Afrika Mashariki, na kocha mkuu wa KCCA amesema ana imani na kikosi chake licha ya kuwa Al Ahly wanapewa nafasi kubwa.

  Katika mechi ya kwanza ya hatua ya makundi iliyopigwa nchini Botswana, KCCA walipoteza kwa goli 1-0 dhidi ya Township Rollers.

  Mechi nyingine ya kundi hilo itazikutanisha Township Rollers ambayo inaongoza kundi B kwa kuwa na pointi 3, na Esperance ya Tunisia ambayo ina pointi 1 baada ya kutoka sare kwenye mechi kwanza dhidi ya Al Ahly.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako