• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kombe la Shirikisho: Rayon Sport ya Rwanda yawasili Dar es Salaam kucheza Yanga ya Tanzania

  (GMT+08:00) 2018-05-15 10:09:25

  Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda imewasili nchini Tanzania kwa ajili ya kuwakabili wenyeji Young Africans kwenye mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Mei 16 mjini Dar es Salaam.

  Katika mchezo wake wa kwanza Rayon ilipata sare ya goli 1-1 dhidi ya Gor Mahia FC ya Kenya, na wenzao Young Africans wakipoteza kwa magoli 4-0 dhidi ya USM Algiers ya Algeria.

  Mechi nyingine ya kundi D itapigwa mjini Nairobi, ambapo USM Algiers ambao wanaongoza kundi D, na tayari wamewasili nchini Kenya, watacheza na wenyeji wao Gor Mahia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako