• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sababu zinazochangia meno ya watoto kutoboka na kuoza

  (GMT+08:00) 2018-05-15 10:53:59

  Afya ya kinywa ni muhimu hata kwa mtoto mchanga ambaye hana meno kinywani mwake. Ingawa meno ya mtoto mchanga huanza kuonekana miezi sita baada ya kuzuliwa, mzazi anashauriwa kuanza kusafisha kinywa chake siku chache baada ya kuzaliwa kwa kufuta fizi zake kwa kitambaa kisafi.

  Mpana meno yam toto mchanga yaanze kuonekana yanaweza kupata maambukizi endapo kinywa kitakuwa hakitunzwi vyema. Wakati yakiota, yanaweza yakaanza kutoboka hivyo ni vizuri kuanza kumzoesha mtoto husika usafi wa kinywa na meno.

  Kuanza kutunza meno yam toto tangu anapokua mchanga huweza kumkinga na kutoboka kwa meno na magonjwa mengine ya kinywa kwa miaka mingi ijayo. Pindi mtoto anapozaliwa, taya zake zimeshabeba meno yote 20 ya utotoni.

  Anza kusafisha kinywa cha mtoto wako siku chache baada ya kuzaliwa kwa kufuta fizi zake kwa kitamba kisafi. Meno ya mbele ya utotoni huweza kujitokeza miezi sita baada ya kuzaliwa ingawa baadhi ya watoto kuchelewa kuota meno mpaka miezi 12 au 14.

  Mpaka ujiridhishe kuwa mwanao anaweza kupiga mswaki mwenyewe, endelea kumsaidia kupiga mswaki mara mbili kwa siku kwa kutumia mswaki wa watoto pamoja na dawa ya meno yenye madini ya floridi.

  Kwa mtoto wenye umri wa chini ya miaka mitatu, wazazi ama walezi wanatakiwa waanze kumpigisha mswaki mara tu meno yanapoanza kutokeza kinywani. Mswaki huo unatakiwa uwe mdogo na dawa ya meno yenye madini ya floridi ukubwa wa punje ya mchele.

  Upigaji wa mswaki unapaswa kufanywa kwa umakini asubuhi baada ya kifungua kinywa na usiku kabla ya kulala. Mzazi anatakiwa akikishe mtoto hamezi dawa ya meno inayotumika wakati wa kusafisha kinywa na meno, mtoto aiteme yote na kusukutua kwa maji safi.

  Kwa watoto wa umri wa kati ya miaka mitatu mpaka sita, wakati wa kupiga mswaki, mzazi anatakiwa ahakikishe dawa ya meno inayotumika ina madini ya floridi na ukubwa wa punje ya harage.

  Kwa kawaida, meno ya utotoni yanapoanza kujitokeza miezi sita mpaka mwaka mmoja baada ya kuzaliwa, baadhi ya watoto huvimba na kuhisi maumivu kwenye fizi.

  Inashauriwa, hali hii inapotokea, pitisha taratibu kidole ama kitambaa kisafi ili kutuliza hali hiyo. Watoto wengi wafikapo umri wa miaka mitatu, huwa na meno yote 20 ya utotoni.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako