• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Afrika yahimizwa kukuza sera ya biashara huru

    (GMT+08:00) 2018-05-15 18:14:55
    Afrika imetakiwa kufungua milango kwa biashara baina ya nchi za bara hilo ili kusaidia ukuaji wa haraka wa uchumi.

    Naibu Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika Thomas Kwesi Quartey, amesema mjini Addis Ababa kuwa Eneo huru la Biashara la Bara la Afrika ni muhimu katika kukuza Pato la bara hilo.

    Alisema wakati biashara ya -Afrika inapokua kwa asilimia 2, Pato la jumla linakua kwa asilimia 10.

    Alidokeza kwamba kulingana na utabiri wa utendaji wa eneo huru la kibiashara la Afrika ni dhahiri kwamba ya litaongeza matumizi ya wanunuzi kwa dola trilioni 1.4 ifikapo 2020.

    Vivyo hivyo, itaongeza biashara ya Afrika kwa kiasi cha dola bilioni 35 kwa mwaka, au asilimia 52 ifikapo mwaka wa 2022.

    Tayari nchi 44 kati ya nchi 55 za Umoja wa Afrika zimesaini makubaliano ya kuanzisha soko huru huku Nigeria na Afrika Kusini, zikitarajiwa kujiunga baadaye.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako