• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • WHO kufanya majaribio ya chanjo ya Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

  (GMT+08:00) 2018-05-15 19:32:33

  Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Afya Duniani WHO Bw. Tedros Ghebreyesus amesema Shirika hilo linapanga kufanya majaribio ya chanjo ya Ebola katika eneo la kaskazini magharibi mwa DRC ambapo mlipuko wa ugonjwa huo umetokea.

  Habari zinasema kuwa chanjo hiyo ilifanyiwa uchunguzi na idara ya afya ya jamii ya Canada na kutengenezwa na kampuni ya Merck&Co ya Marekani. Jaribio lililofanywa nchini Guniea lilioneshwa kuwa kiwango cha mafanikio cha chanjo hiyo kitafikia asilimia 100.

  Bw. Ghebreyesus amesema, chanjo hiyo inatarajiwa kuwasili nchini DRC jumatano au alhamis wiki hii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako