• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sifa tatu za kipekee za chombo cha uchunguzi cha Mars

  (GMT+08:00) 2018-05-16 09:31:47

  Chombo cha uchunguzi cha Mars cha Insight kilirushwa tarehe 5 na Idara ya anga ya juu ya Marekani NASA. Ingawa chombo hiki si chombo cha kwanza kutembelea Mars, lakini kina sifa tatu za kipekee.

  Kwanza, chombo cha Insight kitakuwa cha kwanza kufanya utafiti wa Mars kwa kina. Ingawa kabla ya hapo chombo cha uchunguzi cha Opportunity kiliwahi kupiga picha za Mars, na chombo cha Curiosity kiliwahi kukusanya sampuli, lakini binadamu bado wanajua mambo machache kuhusu sayari hiyo. Chombo cha Insight kitakaa kwenye Mars na kutafiti mambo kuhusu sehemu ya ndani ya sayari hiyo, ikiwemo ukubwa na muundo wa kiini cha sayari hiyo, joto la ndani ya sayari na matetemeko ya ardhi.

  Pili, chombo hiki kina vifaa mbalimbali, na vyombo vya kupima matetemeko ya ardhi na joto la ndani ya sayari vitawekwa kwenye ardhi ya sayari hiyo na kudumu.

  Tatu, urushaji wa chombo hiki umevunja rekodi. Kabla ya hapo vyombo vya uchunguzi wa anga ya juu vya NASA vyote vilirushwa katika pwani ya mashariki ya Marekani halafu kuelekea mashariki, kwani dunia inazunguka kutoka magharibi kwenda mashariki, na urushaji unaoelekea mashariki utasaidiwa na mwendo kasi wa kujizungusha kwa dunia. Lakini chombo cha Insight kilirushwa angani katika pwani ya magharibi, kwa sababu chombo hiki ni kidogo, kinaweza kurushwa angani na roketi ya Atlas V-401, kuelekea upande wa kusini halafu kwenda Mars.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako