• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Chombo cha anga ya juu cha Dragon kinachobeba panya charudi duniani

  (GMT+08:00) 2018-05-16 09:32:40

  Chombo kinachobeba mizigo cha anga ya juu cha Dragon kilichorushwa na kampuni ya SpaceX kilirudi duniani tarehe 5 kutoka kituo cha anga ya juu cha kimataifa. Chombo hiki kimebeba zaidi ya tani 1.8 za mizigo na sampuli za majaribio ya kisayansi.

  Kampuni ya SpaceX imesema baada ya kutenganishwa na kituo cha anga ya juu cha kimataifa, chombo hiki kiliruka kwa saa 5 na nusu, na kuanguka kwenye bahari ya Pasifiki. Chombo hiki kilirudishwa na kampuni hiyo baadaye.

  Panya waliokaa kwenye kituo cha anga ya juu kwa muda kadhaa wamerudi duniani kwa kupanda chombo hiki. Wanasayansi wanatarajia kutafiti mabadiliko ya mifupa ya panya katika mazingira yanayokosa nguvu ya mvutano wa dunia. Sampuli muhimu za kiviumbe zilizohifadhiwa kwenye friji zikiwemo za mimea, wadudu na mkusanyiko wa seli za binadamu pia zimeletwa duniani.

  Chombo hiki kilirushwa angani tarehe 2 Aprili kwa roketi ya Falcon 9, na kupeleka tani 2.63 za vitu na vifaa vya utafiti kwenda kituo cha anga ya juu cha kimataifa. Hii ni mara ya 14 kwa kampuni hiyo kufanya kazi ya kupeleka mizigo kwa idara ya anga ya juu ya Marekani NASA.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako