• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Taasisi za Confucius zapiga hatua kubwa barani Afrika

  (GMT+08:00) 2018-05-16 17:41:43

  Tangu taasisi ya kwanza ya Confucius ya China barani Afrika ianzishwe katika Chuo Kikuu cha Nairobi, Kenya, taasisi hizi za kufundisha lugha ya kichina zimepata mafanikio makubwa barani humo. Mkutano wa taasisi za Confucius barani Afrika umefanyika hivi karibuni huko Maputo, Msumbiji. Kwenye mkutano huo mkuu wa ofisi ya kueneza lugha ya kichina duniani ya wizara ya elimu ya China Bw. Ma Jianfei amesema, taasisi za Confucius barani Afrika zimepiga hatua kubwa.

  Hadi sasa, China imeanzisha taasisi 54 na madarasa 30 ya Confucius barani Afrika, na kuwafundisha wanafunzi zaidi ya milioni 1.4. Mkuu wa ofisi ya kueneza lugha ya kichina duniani ya wizara ya elimu ya China Bw. Ma Jianfei anasema,

  "Mwaka jana idadi ya wanafunzi waliojiandikisha kusoma katika taasisi za Confucius barani Afrika ilifikia laki 1.5. Katika mwaka huo, taasisi hizo ziliandaa matamasha ya utamaduni na semina zaidi ya 2,500, ambazo ziliwavutia watu zaidi ya laki 8.4."

  Bw. Ma amesema hadi sasa nchi 14 za Afrika zimeweka mafunzo ya lugha ya kichina katika mfumo wao wa elimu kutokana na uungaji mkono wa taasisi za Confucius, na vyuo vikuu vya nchi 21 vyenye taasisi ya Confucius vimeanzisha kozi za lugha ya kichina. Taasisi za Confucius pia zimeshirikiana na idara za serikali na huduma za jamii kutoa mafunzo ya lugha ya kichina kwa watumishi wao. Bw. Ma amesema taasisi za Confucius barani Afrika si kama tu zinafundisha lugha, bali pia zinatoa mafunzo ya ufundi. Anasema,

  "Kwa Mfano nchini Ethiopia, taasisi ya Confucius inatoa mafunzo kuhusu teknolojia ya umeme, magari na malori, na taasisi ya Confucius nchini Libya inawafundisha wanafunzi ufundi wa kutengeneza vifaa kwa kutumia mianzi."

  Takwimu zinaonesha kuwa tangu mwaka 2012, wastani wa kila mwaka wa ongezeko la idadi ya wanafunzi katika taasisi za Confucius barani Afrika ni asilimia 36. Bw. Ma Jianfei anasema,

  "Taasisi za Confucius barani Afrika zinazingatia matumizi ya walimu wenyeji na mahitaji halisi ya wanafunzi. Mwaka jana taasisi hizo zilifundisha walimu 1,500 wenyeji, na kuwaajiri walimu karibu 100 wa kienyeji. Aidha, taasisi hizo zinazingatia mahitaji halisi ya wanafunzi. Kwa mfano hivi sasa mashirika mengi ya China yameingia barani Afrika, na taasisi za Confucius zinaweza kufundisha wanafunzi wanaolingana na vigezo vya ajira vya mashirika hayo."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako