• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania-Serikali imefuta ada na tozo kwa wakulima wa miwa,pamba,chai na kahawa

  (GMT+08:00) 2018-05-16 19:31:53

  Serikali ya Tanzania imeshusha neema kwa wakulima wa miwa,pamba ,chai na kahawa nchini baada ya jana kutangaza kufuta ada na tozo 21 zilizokuwa kero na kikwazo kwa maendeleo yao.

  Katika kuhakikisha upatikanaji wa pembejeo unakuwa wa uhakika na kwa bei nafuu,imependekeza kufuta tozo tano kwenye uzalishaji mbegu huku ikipendekeza kufuta tozo zingine sita kwa lengo la kuimarisha maendeleo ya ushirika.

  Imeelezwa kuwa hatua hiyo ya serikali ni sehemu ya mkakati wa kumaliza kero zinazowakabili wakulima ambao Rais John Pombe Magufuli amekuwa akiusisitiza.

  Kuhakikisha mkakati huo unatekelezwa,serikali imesema imefanya marekebisho ya kanuni na sheria zilizoanzisha tozo na ada husika,hivyo utekelezaji wake uzingatiwe na hatua kali zitachukuliwa kwa watakaokiuka.

  Uuamuzi huo wa serikali ulitangazwa jana bungeni jijini Dodoma na Waziri wa Kilimo ,Dk Charles Tizeba,alipowasilisha hotuba ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka ujao wa fedha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako