• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mchezo wa Mpira wa Mikono: Timu ya vijana ya Rwanda yapata ushindi mfululizo, kucheza na Burundi leo

  (GMT+08:00) 2018-05-17 08:39:49

  Timu ya taifa ya vijana ya Rwanda ya vijana chini ya umri wa miaka 20 jana imeshinda kwa alama 55-8 na Sudan na kuendeleza rekodi yake ya kutofungwa kwenye mashindano ya kimataifa yanayoendelea mjini Kampala, nchini Uganda.

  Katika mechi hiyo Samuel Mbesutunguwe aliibuka mchezaji bora, na mfungaji bora alipopata alama 14.

  Huu ulikuwa ushindi wa pili kwa timu hiyo, kwani siku ya jumatatu ilifanikiwa kushinda mechi nyingine dhidi ya wenyeji Uganda kwa alama 30-29 na kocha mkuu wa timu hiyo Anaclet Bagirisha, akisema matokeo hayo ni mazuri lakini jitihada zaidi zinahitajika.

  Timu hiyo icheza tena leo mechi ya tatu ya hatua ya makundi dhidi ya majirani zao Burundi, na katika kundi B la mashindano hayo ya wiki moja, Rwanda iko pamoja na timu za Burundi, Somalia na wenyeji Uganda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako