• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wang Yi azitaka pande husika zifanye juhudi sambamba kwenye suala la peninsula ya Korea

  (GMT+08:00) 2018-05-17 09:42:41

  Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi ambaye yuko ziarani nchini Ufaransa, ametoa mwito kwa pande zote husika kufanya juhudi sambamba badala ya kwenda kinyume kwenye suala la nyuklia la peninsula ya Korea.

  Amesema suala la nyuklia la Peninsula ya Korea ni suala sugu lililodumu kwa muda mrefu, na utatuzi wake unahitaji juhudi za pamoja, haswa kuepusha kutokea kwa hali ambayo upande mmoja umelegeza msimamo huku mwingine ukiimarisha msimamo.

  Pia amesisitiza kuwa hali iliyopo sasa katika Peninsula hiyo haikupatikana kirahisi, na pande zote hususan Marekani zinapaswa kuthamini fursa ya amani iliyopo, na kuwa mhimizaji na wala sio mhujumu wa mchakato wa amani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako