• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Maonesho ya 15 ya kimataifa ya China ya filamu na tamthiliya yafunguliwa

  (GMT+08:00) 2018-05-17 17:52:43

  Maonesho ya 15 ya kimataifa ya China ya filamu na tamthiliya yamefunguliwa leo hapa Beijing, na kuyashirikisha mashirika zaidi ya 300 kutoka nchi zaidi ya 50.

  Maonesho ya 15 ya kimataifa ya China ya filamu na tamthiliya yameandaliwa na Shirika kuu la Radio na Televisheni la China. Meneja mkuu wa shirika la biashara za vipindi vya radio, filamu na tamthilia Bi Shen Jianing anasema,

  "Hii ni mara ya kwanza kwa maonesho hayo kuweka maeneo maalumu mbalimbali ya VR, vyombo vipya vya habari, filamu na tamthiliya zilizotafsiriwa, na ubalozi. "

  Mhariri mkuu wa kipindi cha "wakati wa China" cha shirika la habari la Dove la Uingereza Bw. Gordon amesema kipindi chao cha "wakati wa China" pia kinaoneshwa na televisheni ya Sky na kufikishwa kwa watazamaji wa Uingereza zaidi ya milioni 12. Anasema,

  "Kipindi chetu kinahusu mambo ya mashirika na nchi zinazoshiriki kwenye pendekezo la 'Ukanda Mmoja na Njia Moja'. Tunatoa vipindi kuhusu China nchini Uingereza, vinavyopendwa sana na watazamaji. Vilevile tunatumai kutoa vipindi vya Uingereza kwa watazamaji wa China, wanaovutiwa na utamaduni wetu."

  Filamu na tamthiliya ni njia bora ya mawasiliano ya utamaduni. Bw. Redrigo Lommerte kutoka Brazil amesema anapenda tamthiliya za China, na kutarajia kuweza kuangalia tamthiliya nyingi zaidi za China nchini Brazil, ili kuielewa zaidi China na utamaduni wake. Anasema,

  "Napenda kutazama filamu na tamthilia za China aina za Kongfu, uhalifu, na za kutisha, ambazo ni vigumu kuzipata nchini kwetu. Hatujui mambo mengi kuhusu China kama vile maisha ya watu, utamaduni na lugha. Vipindi vya televisheni vinatuwezesha kuelewa jinsi jamii ya China inavyoendelea."

  Ili watu wa nchi za nje waelewe zaidi mambo ya China, China ilianzisha mradi wa Thieta ya China. Hadi sasa ofisi ya tafsiri za filamu na tamthilia kwa lugha mbalimbali ya Shirika kuu la Radio na Televisheni la China imesaini makubaliano na mashirika ya nchi zaidi ya 30 za mabara ya Asia, Afrika, Ulaya na Oceania. Kwa mujibu wa makubaliano hayo, filamu na tamthiliya za China zinatolewa kila wakati maalumu kwa watazamaji wa nchi hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako