• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Naibu waziri mkuu wa China akutana na wabunge muhimu wa Marekani kujadili uhusiano kati ya pande hizo

  (GMT+08:00) 2018-05-17 19:20:06

  Naibu waziri mkuu wa China na mjumbe maalum wa rais wa China Bw. Liu He amekutana na aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani Henry Kissinger na baadhi ya wabunge muhimu wa Marekani kujadili uhusiano wa pande hizo mbili.

  Liu aliwasili Marekani jumanne mchana kwa ajili ya majadiliano ya kiuchumi na kibiashara na upande wa Marekani. Alipokutana na Kissinger, Liu alimpongeza mwanadiplomasia huyo wa siku nyingi kwa ahadi yake ya muda mrefu ya kudumisha urafiki kati ya China na Marekani. Amesema atatafiti suluhisho sahihi la suala la biashara ili kuhakikisha maendeleo mazuri ya uhusiano wa kibiashara kati ya China na Marekani.

  Kwa upande wake, Kissinger amesema kushughulikia uhusiano wa China na Marekani kunahitaji mtazamo wa kimkakati kwa kuwa kunahusisha amani na ustawi wa dunia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako