• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Vyama vya vya ushirika Kenya vyaitaka serikali kusambaza fedha za maendeleo kwa umma

    (GMT+08:00) 2018-05-18 19:07:01

    Vyama vya vya ushirika nchini Kenya vimeitaka serikali kujaribu kusambaza fedha za maendeleo kwa umma kwa vyama vyao kwa minajili ya kuwapa wahusika mashinani fursa ya kujiendeleza.

    Mwenyekiti wa Urithi Premier Sacco Bw Pius Thuku alipendekeza Jumatano kwamba fedha za Uwezo kwa Vijana na Wanawake ziwasilishwe kwa vyama vya ushirika vinavyoendesha biashara zao kwa uwazi.Amesema wangetaka kufanya ushirikiano wa karibu na serikali kwa minajili ya kusambaziwa fedha za Uwezo, Vijana na wanawake ili nao wazisambaze kwa wananchi waliopo mashinani.

    Amesema wao kama chama cha ushirika wanajumuika na wananchi katika mashinani na iwapo watafanya uelewano na serikali kusambaza fedha hizo bila shaka wananchi wa mashinani watapata nafasi ya kupokea fedha hizo kwa urahisi. Amesisitiza kuwa vyama ambavyo vimejiendeleza na vinahudumia wananchi kwa uwazi bila ubaguzi vinastahili kupewa jukumu hilo la kusambaza fedha hizo za serikali kwa wananchi. Amewahimiza wananchi kujiunga na vyama vya ushirika vilivyojiendeleza vyema ili kunufaika pakubwa na mikopo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako