• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kutoa mafunzo kuziba pengo la wataalamu wa kutengeneza bomba la mafuta

    (GMT+08:00) 2018-05-18 19:08:43

    Kenya itaanza kutoa mafunzo ya uchomaji vyuma ili kuziba pengo ambalo limepelekea kuajiri wataalamu kutoka nchi za China, Nigeria na Lebanon kwenye mradi wake wa kujenga bomba la mafuta.

    Benki ya dunia inatarajiwa kufadhili mafunzo hayo si8ku chache tu kabla ya uzinduzi wa ujenzi wa bomba la mafuta kati ya Nairobi na Mombasa lenye gharama ya shilingi bilioni 43. Bomba lingine la mafuta ni la kilomita 820 kutoka Lokichar hadi lamu ambalo linatarajiwa kukamilika ifikapo mwaka wa 2021. Taarifa hiyo ya serikali inakuja wakati ambapo serikali tayari imeajiri wataalamu 50 kutoka nchi za Nigeria, Lebanon na China baada ya kuona kuna upungufu wa wataalamu kwenye sekta hiyo. Kampuni ya Global consultancy firm imepatiwa kandarasi kutoa mafunzo hayo kwa wafanya kazi 12 wa kampuni ya mafuta ya Kenya KPLC. KPLC imesema ina wataalam 3 pekee wenye ujuzi wa kutengeneza mabomba ya mafuta.Hii pia imepelekea serikali kuanza kuboresha taasisi za kutoa mafunzo ya kiufundi hapa nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako