• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China kuendelea kujihusisha na mambo ya usimamizi wa afya duniani

  (GMT+08:00) 2018-05-21 19:29:41

   

  Mkutano wa 71 wa afya duniani WHO umefunguliwa leo mjini Geneva, ambapo kiongozi wa ujumbe wa China kwenye mkutano huo, ambaye ni mkurugenzi wa Kamati ya afya ya China Bw. Ma Xiaowei amesema, China imekuwa ikiweka mkazo katika kuhakikisha afya ya umma na kunufaisha zaidi maisha ya watu, kujiunga na mambo ya usimamizi wa afya duniani, na kuchangia katika afya ya binadamu kwa busara na nguvu ya China.

  Mkutano wa afya duniani ni mkutano mkubwa zaidi wa WHO ambao unaofanyika kila baada ya mwaka mmoja na kujadili masuala muhimu ya afya duniani. Mkurugenzi wa Kamati ya afya ya China Bw. Ma Xiaowei ameongoza ujumbe wa serikali ya China kuhudhuria mkutano wa mwaka huu. Amesema kwenye mkutano na waandishi wa habari kuwa, China imeliweka suala la afya kwenye mikakati ya taifa, na kuanzisha ushirikiano na mashirika mbalimbali ya kimataifa ikiwemo WHO, ili kuchangia katika kazi ya kuboresha afya ya watu duniani. Bw. Ma Xiaowei anasema:

  "China ikiwa nchi kubwa inayoendelea duniani, imetoa mchango muhimu katika kutafuta uzoefu wenye ufanisi katika usimamizi wa mambo ya afya, na kubadilshana uzoefu huo na nchi nyingine."

  Katika mkutano huo Bw. Ma Xiaowei amefahamisha uzoefu wenye umaalumu wa China ukiwa ni pamoja na harakati ya kuwahamasisha wananchi kujiunga na mambo ya afya kwa moyo wa uzalendo, utaratibu wa kupambana na maradhi unaozingatia kinga zaidi, mtandao wa afya na matibabu kwa wananchi unaohusisha maeneo makubwa zaidi duniani, na utoaji wa huduma kwa akina mama na watoto. Amesisitiza kuwa hatua hizo za China zimetoa uzoefu mzuri kwa usimamizi wa mambo ya afya duniani.

  Mbali na kazi hizo, katika miaka mingi iliyopita, China imekuwa ikitoa msaada kwa nchi zinazoendelea kushughulikia mambo ya afya, kuongoza operesheni ya kimataifa ya utoaji wa misaada ya dharura. Tokea mwaka 1963, China imetuma watu elfu 25 kwa nchi zinazoendelea, kutoa matibabu kwa wagonjwa milioni 280. Bw. Ma Xiaowei akizungumzia mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola uliotokea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, amesema wakati ugonjwa huo ulipoibuka katika nchi za Afrika Magharibi mwaka 2014, China ilituma wafanyakazi zaidi ya 1,200 wa matibabu katika nchi hizo ili kusaidia kupambana na ugonjwa huo, na kutoa mchango mkubwa kwa ajili ya udhibiti wa ugonjwa huo, akisema:

  "China inafuatilia sana mlipuko mpya wa ugonjwa wa Ebola, na taarifa kuhusiana na ugonjwa huo. China itajihusisha kwa juhudi kubwa kazi ya kukinga na kudhibiti ugonjwa wa Ebola, na kubadilishana uzoefu uliopatikana katika kupambana na ugonjwa huo mwaka 2014 na jumuiya ya kimataifa."

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako