• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chanjo ya Ebola yaanza kutolewa DRC

    (GMT+08:00) 2018-05-22 10:29:36

    Shirila la Afya Duniani WHO limesema chanjo ya Ebola imeanza kutolewa kwa watu wenye hatari kubwa ya kuambukizwa homa hiyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC, ikiwa ni hatua muhimu ya kudhibiti mlipuko wa sasa wa homa hiyo.

    WHO limesema limeipatia DRC chanjo zaidi ya 7,500 kwa ajili ya watu wa mkoa wa Ikweta, ulioko kaskazini magharibi mwa nchi hiyo, ambako watu 26 wamefariki dunia kutokana na homa hiyo mpaka Ijumaa iliyopita. Mkurugenzi mkuu wa WHO Dk. Tedros Ghebreyesus amesema kutoa chanjo kutakuwa njia kuu ya kudhibiti mlipuko wa homa hiyo.

    Wakati huo huo, idara ya afya ya Ghana GHS imeikanusha ripoti kuhusu kugunduliwa kwa Ebola nchini humo, na kwamba serikali ya Ghana inajaribu kuzuia habari hiyo. Idara hiyo imetoa taarifa ikisisitiza hakuna virusi vya Ebola nchini Ghana na habari hiyo haiendani na hali halisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako