• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Trump asema mkutano wake na Kim unaweza kuahirishwa

    (GMT+08:00) 2018-05-23 10:06:05

    Rais Donald Trump wa Marekani amesema mkutano unaotarajiwa kufanyika Juni, 12 nchini Singapore kati yake na kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un unaweza kuahirishwa.

    Rais Trump amesema hayo alipozungumza na waandishi wa habari katika Ikulu ya Marekani wakati wa mkutano wake na rais Moon Jae-in wa Korea Kusini aliyekuwa ziarani nchini Marekani.

    Wiki iliyopita Korea Kaskazini ilionya kuwa itafikiria tena kama itashiriki kwenye mkutano wa Singapore kama Marekani "inataka tu kuishinikiza nchi hiyo kuacha silaha zake za nyuklia."

    Korea Kaskazini iliahirisha mazungumzo kati yake na Korea Kusini Jumatano iliyopita ili kupinga mazoezi makubwa ya kijeshi ya pamoja kati ya Marekani na Korea Kusini na kuitaka Korea Kusini kusimamisha mazoezi hayo.

    Habari nyingine kutoka Wizara ya Korea Kusini inayoshughulikia masuala ya muungano wa Korea mbili zinasema Korea Kaskazini imepokea orodha ya wanahabari wanane wa Korea Kusini na kuwaruhusu kutoa ripoti kuhusu eneo lake la majaribio la nyulia la Punggye-ri linalotarajiwa kuharibiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako