• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Masumbwi, Tanzania: Serikali yakubali kufutwa kwa vyama vinavyochochea vurugu

  (GMT+08:00) 2018-05-23 10:59:51

  Serikali ya Tanzania, imetoa mamlaka kwa msajili wa vyama vya michezo kuvifutia usajili vyama viwili vya mchezo wa masumbwi vya kulipwa, TPBO na PST endapo ataona vinakiuka kanuni za uratibu na uendeshaji wa mchezo huo, na kwa kufanya kinyume na matakwa ya nchi.

  Mamlaka hiyo imetolewa na Waziri wa Michezo wa Tanzania, Harrison Mwakyembe, baada ya mwenyekiti wa kamati ya kusimamia mchezo wa ngumi nchini Tanzania, kueleza kuwa wanashindwa kutekeleza majukumu yao kutokana na vikwazo walivyowekewa na viongozi hao wa TPBO na PST, ambao ni Yassin Abdallah, na Emmanuel Mlundwa.

  Zaidi waziri Mwakyembe amesema serikali imesikitishwa na taarifa kuwa viongozi hao wamekuwa wakifanya vurugu, na wakati mwingine kuidhihaki serikali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako