• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka, Zanzibar: ZFA yazungumzia mkanganyiko uliojitokeza wa kanuni za uhamisho wa wachezaji

    (GMT+08:00) 2018-05-23 11:00:12

    Chama cha Soka Zanzibar ZFA, kimekiri kuwepo kwa mkanganyiko wa kanuni ya kusimamia ligi uliochangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa malalamiko mengi ya wachezaji waliotoka Tanzania Bara.

    Akizungumza na gazeti moja mjini Unguja, Katibu wa ZFA Mohammed Ali 'Tedy' amesema kuwa mambo mengi yaliyojitokeza katika ligi Kuu ya Zanzibar Kanda ya Unguja yalitokana na kanuni ya sasa.

    Alisema kuwa katika kanuni hiyo kipengele cha wachezaji kutoka bara, haikufafanua vizuri na kusababisha kuwepo na malalamiko mengi ya rufaa, kwani kanuni hiyo haipo wazi kuelezea juu ya uhamisho unaotakiwa kufanywa kwa mchezaji anayetoka Tanzania bara.

    Hata hivyo alisema kuwa ZFA katika kipindi hicho ilikuwa ikiidhinisha wachezaji ambao uhamisho wao na usajili haukufanyika kwa mujibu wa taratibu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako