• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa China na Marekani wakutana

    (GMT+08:00) 2018-05-24 10:04:17

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amekutana na mwenzake wa Marekani Bw. Mike Pompeo mjini Washington na kubadilishana naye maoni kuhusu uhusiano kati ya nchi hizo mbili na masuala wanayofuatilia kwa pamoja.

    Bw. Wang amesema ni muhimu kudumisha uhusiano mzuri kati ya China na Marekani, kuimarisha ushirikiano wa kusaidiana, kutatua tofauti na masuala kwa njia mwafaka na kupanua ushirikiano katika masuala ya kikanda na kimataifa.

    Kwa upande wake Bw. Pompeo amesema Marekani inapenda kushirikiana zaidi na China, na kwamba rais Donald Trump anathamini sana uhusiano mzuri wa kikazi na urafiki binafsi kati yake na rais Xi Jinping wa China. Ameongeza kuwa katika suala la Taiwan, Marekani inashikilia msimamo wa kuwepo kwa China moja. Katika suala la uchumi na biashara, amesema hivi karibuni vikosi kazi vya kiuchumi vya Marekani na China vilifanya majadiliano ya kiujenzi na ameeleza matumaini yake kuwa nchi hizo mbili zinaweza kubainisha na kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa na kuwanufaisha wananchi wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako