• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema kuweka vifaa vya ulinzi katika visiwa vya Bahari ya Kusini ya China ni kitendo halali

    (GMT+08:00) 2018-05-24 10:04:46

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema China inafanya shughuli za kiujenzi katika visiwa vyake kwenye Bahari ya Kusini ya China, ambazo nyingi zinahusu vifaa vya kiraia, na pia kuna vifaa vya ulinzi vya lazima.

    Bw. Wang ameyasema hayo alipoulizwa na mwandishi wa habari wa Marekani kuhusu kinachotajwa kuwa mambo ya kijeshi yanayofanywa na China katika Bahari ya Kusini ya China. Amesema shughuli hizo ni kutekeleza haki ya kujilinda kwa mujibu wa sheria ya kimataifa, na hazihusishi mambo ya kijeshi, hali ambayo inafanana na Marekani kuweka vifaa vya kiujenzi katika kisiwa cha Guam na Hawaii, lakini ukubwa wa uwekaji wa China ni mdogo ikilinganishwa na ule wa Marekani.

    Wakati huohuo, alipozungumzia Wizara ya Ulinzi ya Marekani kuacha kulialika jeshi la China kushiriki kwenye mazoezi ya kijeshi ya pamoja katika Bahari ya Pasifiki RIMPAC, Bw. Wang amesema uamuzi huo sio wa kiujenzi, na wala sio wa makini, na hausaidii kuzidisha maelewano na kuaminiana kati ya China na Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako