• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Chama tawala Afrika Kusini chalaani mfululizo wa mauaji ya kisiasa

    (GMT+08:00) 2018-05-24 10:24:12

    Chama tawala cha Afrika Kusini ANC kimelaani mfululizo wa mauaji ya kisiasa yanayotokea katika Jimbo la KwaZul Natal.

    Kauli hiyo imetolewa baada ya mwenyekiti wa Kundi la Shack Dwellers Bw S'fiso Ngcobo kuuawa Jumanne wilayani Mariannhill, magharibi mwa mji wa Durban na, kiongizi mwingine wa kundi hilo Bw Ndumiso Muguni kushambuliwa kwa risasi mjini Durban na sasa yuko mahututi.

    Msemaji wa Chama cha ANC Bw Pule Mabe amesema chama hicho kinalaani vikali mauaji hayo yenye malengo ya kisiasa, na kwamba chama cha ANC kitaipa kipaumbele kazi ya kupambana na uhalifu.

    Mbali na hayo profesa Gregory Kamwendo wa Chuo Kikuu wa Zululand aliuawa kwa kupigwa risasi alipokuwa anarudi nyumbani mjini Empangeni, na madhumuni ya mauaji hayo bado hayajulikani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako