• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa Umoja wa Mataifa asema China inaweza kuisaidia Afrika kunufaika na eneo la biashara huria

    (GMT+08:00) 2018-05-24 10:47:27

    Ofisa wa Umoja wa Mataifa amesema China inaweza kulisaidia bara la Afrika kunufaika na eneo la biashara huria.

    Mkurugenzi wa Kitengo cha Maendeleo ya Uwezo cha Kamati ya uchumi wa Afrika ya Umoja wa mataifa UNECA Bw. Stephen Karingi alisema jana mjini Nairobi kuwa kama Afrika ikitaka kunufaika zaidi na utaratibu wa biashara huria, itahitaji uwekezaji mpya katika miundo mbinu, raslimali watu na viwanda. Amesema China ina rasilimali hizi zote ambazo zinaweza kutumiwa barani Afrika, ili kulisaidia eneo la biashara huria kuwa na manufaa zaidi, na kwamba kuna fursa nyingi ambazo China inaweza kushirikiana na Afrika kuliwezesha bara hilo kupata manufaa halisi yanayotokana na biashara huria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako