• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Ulaya wasisitiza kufanya ushirikiano na Marekani kwenye sekta ya usalama

    (GMT+08:00) 2018-05-24 18:35:08

    Mkutano wa siku mbili wa mawaziri wa Umoja wa Ulaya na Marekani kuhusu suala la usalama umemalizika jana huko Sofia nchini Bulgaria.

    Taarifa ya pamoja iliyotolewa na mkutano huo imesisitiza kuwa, pande hizo mbili zitaendelea kufanya ushirikiano kwenye kupambana na ugaidi na kubadilishana taarifa za kipepelezi, ili kukabiliana na matishio ya usalama.

    Taarifa hiyo imesema, mkutano huo umejadili kupambana na ugaidi, kubadilishana taarifa za kipepelezi, kuzuia msimamo wa siasa kali, kukabiliana na matishio ya usalama wa safari za anga, silaha za kemikali na nyukilia. Vilevile imesisitiza umuhimu kwa Umoja wa Ulaya na Marekani kudumisha ushirikiano wa muda mrefu kati yao kwenye mambo ya ndani na utekelezaji wa sheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako