• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yatajwa kutumia vyema fedha za miradi

    (GMT+08:00) 2018-05-24 19:43:51

    BENKI ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) imeitaja Tanzania kuwa moja ya nchi za Afrika zenye matumizi bora ya fedha zinazofadhiliwa na Benki hiyo kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya miundombinu ya barabara na nishati.

    Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Afrika anayesimamia nchi 7 za Kanda ya Afrika Mashariki, Dk. Nyamajeje Weggoro wakati wa kikao cha Magavana wa nchi za Afrika kwenye Mkutano wa mwaka wa Benki ya AfDB unaoendelea Mjini Busan, Jamhuri ya Korea ya Kusini.

    Dkt. Nyamajeje alisema kuwa changamoto nyingi zinazotokea katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa nchi za Afrika zinatokana na ukosefu wa wataalamu wa fani mbalimbali, jambo linalosababisha miradi mingi kutomalizika kwa wakati hata hivyo Benki ya AfDB inaendelea kuangalia ni jinsi gani inaweza kusaidia kutatua matatizo hayo na kuleta maendeleo chanya kwa nchi za Afrika.

    Tanzania ni wadau wakubwa katika Benki ya AfDB hivyo inanufaika na mikopo nafuu inayotumika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kama vile ujenzi wa Barabara za kiwango cha Lami hususani mkoa wa Tabora na pia miradi ya Nishati ya umeme na maji maeneo mbalimbali nchini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako