• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yafanya juhudi kuiokoa mbuga ya taifa ya Ziwa Manyara

    (GMT+08:00) 2018-05-25 10:22:06

    Serikali ya Tanzania imetangaza mikakati mipya ya kuiokoa mbuga ya taifa ya Ziwa Manyara inayotishiwa kutokana na shughuli za kilimo.

    Mkuu wa Wilaya ya Karatu Bibi Telesia Mahonda, amesema mfumo wa viumbe wa Ziwa Manyara unakabiliwa na tishio, na kama tishio hilo likiachwa mbuga hiyo itatoweka.

    Mkuu huyo wa wilaya amesema wamewaamuru wakulima wa mpunga kwenye vyanzo vya mito kuacha kilimo, na kama wakikaidi amri hiyo wataondolewa kwa nguvu. Lakini amesema kabla ya kuchukua hatua hiyo, wakulima hao watafundishwa mbinu nzuri za kilimo, na watakaokaidi watafikishwa mahakamani.

    Mbuga ya Ziwa Manyara ni nyumbani kwa aina 400 za ndege, watalii wanaotembelea mbuga hiyo wanaweza kuona aina 100 za ndege kwa siku.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako