• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM na Korea Kusini zaeleza kusikitishwa na uamuzi wa Trump kufuta mkutano wake na kiongozi wa Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2018-05-25 10:42:22

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ameeleza wasiwasi wake na uamuzi wa rais Donald Trump wa Marekani wa kufuta mkutano uliopangwa kufanyika mwezi ujao nchini Singapore kati yake na kiongozi mkuu wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un.

    Naye rais Moon Kae-in wa Korea Kusini ameeleza kusikitishwa na uamuzi huo na akaitisha mkutano na maofisa wa serikali yake, ambapo alisisitiza kuwa kuondoa silaha za kinyuklia kwenye Peninsula ya Korea na kujenga amani ya kudumu ni majukumu ya kihistoria, yasiyotakiwa kucheleweshwa wala kuachwa.

    Korea Kaskazini imesema uamuzi huo haulingani na matarajio ya dunia, na iko tayari wakati wowote kukaa na kufanya mazungumzo na Marekani.

    Rais Trump jana alimwandikia barua Bw. Kim akisema mkutano wao hautafanyika kutokana na hasira na uhasama wazi unaoonyeshwa hivi karibuni na Korea Kaskazini. Uamuzi wa Trump umetolewa baada ya Korea Kaskazini kubomoa mahandaki yake kwenye eneo la majaribio la nyuklia huko Punggye-ri kwa kushuhudiwa na wanahabari kutoka China, Russia, Marekani, Uingereza na Korea Kusini walioalikwa na Korea Kaskazini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako